Kigoma Vijana Development Alliance

SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO 2024:

KIVIDEA kama Mdau wa kupinga Ukatili wa kijisia tumeshiriki kikamilifu katika maadhimisho haya.

Tumetoa elimu kwa Vijana kupitia semina zilizoendeshwa katika kituo cha Vijana cha KIVIDEA kuhusiana na;-

– Umuhimu wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia.

– Madhara ya Ukatili wa Kijinsia.

– Namna ya kumsaidia Mhanga wa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.

– Mbinu za kuepuka vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.

– Pamoja na kutoa huduma ya upimaji wa VVU bure kwa Vijana na Wananchi wote.

Pia tumeungana na maafisa kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji,  dawati la jinsia Polisi, Mahakama, Wanasheria, Mh. Diwani kata ya Bangwe, Maafisa maendeleo ya jamii, Viongozi wa dini na viongozi wa Asasi za kiraia katika sherehe za kilele cha siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia zilizofanyika katika ufukwe wa Ziwa Tanganyika (Katonga), kata ya Bangwe, manispaa ya Kigoma Ujiji. Mgeni rasmi alikuwa ni Mh. Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji. 

KUELEKEA MIAKA +30 YA BEIJING; “CHAGUA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA”.

#afyayangumaendeleoyangu, #terredeshommesschweiz, #StopViolenceAgainstWomen, #ActNowToEndViolence, #Vijana, #kividea, #kigoma

kividea

kividea

Leave a Reply

About Us

WE ARE AN ORGANIZATION ADDRESSING POVERTY-RELATED ISSUES SURROUNDING YOUTH IN TANZANIA

Recent Posts

Follow Us

Current Video in our channel