Shirika la KIVIDEA limepata nafasi kushiriki KIKAO CHA ASASI ZINAZOTOA HUDUMA KATIKA ELIMUMSINGI, ambacho kimeanza tarehe16-Agosti mwezi huu- Dodoma. Kikao kimeandaliwa na TAMISEMI.
Mwakilishi wa Shirika la KIVIDEA Ndg. JUSTINA FOKAS : ameshiriki KIKAO CHA ASASI Zinazotoa huduma katika elimumsingi ikiwa na Kauli mbiu” Tupange na Kutekeleza kwa Pamoja Miradi yenye Tija kwa maendeleo ya Elimumsingi” Mgeni Rasmi- Mh. Ummy A Mwalimu,waziri wa nchi OR-TAMISEMI
MALENGO YA KIKAO:
1. Kubadilishana uzoefu wa kazi mbali mbali katika Shule za msingi
2. Kutengeneza mtandao kwa Asasi zilizokutana
3.Kukuza ushirikiano baina ya wadau, wizara ya elimu na Serikali
4.Kuboresha utoaji wa Elimu Nchini.
5.Kuimarisha utekelezaji wa Miradi na huduma kwa shule za msingi
6.Namna asasi zinaendesha shughuli zao na namna wanavyoweza kuosaidia serikali kukuza miundombinu ya shulemsingi
MATARAJIO YA SERIKALI KWA WADAU/ASASI
1. Kubaini mafanikio na changamoto wanazokutana nazo wadau
2. Wadau kuhakikisha wana usajili na vibari
3. Asasi kuwasilisha report za miradi wanayotekeleza
4. kuona namna wadau/asasi wanavyoweza ku expand na kuepusha kulundikana sehem moja
5.Mfumo mzuri wa taarifa ili serikali wajue shughuli wanazofanya wadau
6. vipaumbele vya serikali kwa watoto waliopo mashuleni