Siku ya tarehe 16/10/2021 KiVIDEA ilifanikiwa kufanya hafla fupi ya uzinduzi wa Kituo Cha Vijana ambacho kilifungwa kwa muda ili kuruhusa shughuli za ukarabati wa Kituo kutekelezeka
Tumetekeleza shughuli ya uzinduzi wa Kituo Cha Vijana ambapo shughuli mbalimbali zinazohusisha ikiwemo huduma za Afya ya Uzazi Kama upimaji wa HIV/AIDs, msaada wa kisaikologia na ushauri pamoja na elimu za Afya ya Uzazi, stadi za maisha na Kupinga ukatili zitaendelea kutolewa kwa Vijana wote wa mkoa wa kigoma na nje ya kigoma
Vijana wengi wameweza kutimiza malengo na ndoto zao kupitia Kituo Cha Vijana KIVIDEA ambacho hukutanisha Vijana wakutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa kigoma kwa lengo la kijifunza kutoka kwa Vijana wenzao
Shukrani za kipekee kabisa kwa wafadhiri wetu Terre des hommes schweiz( tdhs) kutusport katika ukarabati wa Kituo Cha Vijana-KIVIDEA