Kuelekea Siku ya Vijana (12/08/2021) – KIVIDEA imejikita katika kuelimisha vijana ili kuondoa ukatili unao wanzunguka katika jamii.
Maana Vijana ni tegemeo kubwa la maendeleo ya Tanzania katika miaka ijayo. Hata hivyo, vijana wa kiume na wa kike hukabiliwa na changamoto nyingi katika ukuaji na kupevuka kwao kutoka ujana
hadi utu uzima hasa katika uhusiano wa kijamii, afya na uchumi.
Vijana tunaweza kutumia njia mbalimbali kila mahali duniani kuelimisha na kushawishi usawa wa kijinsia katika jamii kwa ngazi zote.
Je, tunaweza kufikia dunia yenye usawa wa kijinsia kwa ngazi zote? Kama NDIO ni hatua gani zitumike?