Kwa ufadhili wa terre des hommes schweiz (tdhs), shirika la KIVIDEA kwa kushirikiana na mwezeshaji (Bi. Pendo Samizi) ambaye pia ni Mratibu huduma za Afya na Watoto Manispaa ya Kigoma Ujiji limeendesha mafunzo kwa siku 3 ya utoaji wa huduma rafiki kwa vijana kwa Wahudumu 20 kutoka vituo vya Afya ndani ya manispaa ya Kigoma Ujiji.
Watoa huduma za afya waliopatiwa mafunzo watasaidia vijana wanaotembelea vituo vya afya kwa huduma za afya ya uzazi. Pia watashiriki kutoa huduma za outreach wakati wa matukio ya vijana katika Kituo cha Vijana cha KIVIDEA, kwenye kampeni za kijamii, na kutoa elimu ya afya ya uzazi. Hatua hizi zitasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za rafiki za afya ya uzazi kwa vijana katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji na Wilaya ya Uvinza.
“Yatupasa kuelewa vyema mahitaji ya Vijana kwani hutumia lugha isiyo rasmi kuashiria sehemu ya mwili yenye changamoto/maumivu. Tujiskie fahari kuwahudumia Vijana” – Babu Paschal, Mkurugenzi Mtendaji – KIVIDEA.