Ni muhimu sana kuwapatia elimu vijana ili waweze kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika jamii zao. Hawa ni vijana wakipata elimu na taarifa kuhusu UZAZI WA MPANGO kupitia vipeperushi wakati wa tamasha la kutoa huduma za UZAZI WA MPANGO, UPIMAJI WA UKIMWI na VVU, UKATILI WA KIJINSI na STADI ZA MAISHA. Tamasha lililofanyika katika kata NGURUKA wilaya ya UVINZA. Mradi unafadhiliwa na shirika la TERRE DES HOMMES SCHWEIZ.
Mafunzo juu ya kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa huduma Rafiki za AFYA ZA UZAZI na UZAZI WA MPANGO, yakiendelea leo katika ukumbi wa KIVIDEA. Mafunzo hayo yamewahusisha watendaji wa Kata na Watoa huduma za afya kutoka katika kata mbalimbali za wilaya za UVINZA na MANISPAA YA KIGOMA UJIJI.